IGAD yazindua mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

(CRI Online) Februari 01, 2025

Mamlaka ya Maendeleo ya Serikali za Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) na washirika wake wamezindua mradi wa kuwalinda raia dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, migogoro na kukimbia makazi yao.

Mradi huo uliozinduliwa huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya, unatafuta kukuza ushirikiano kati ya wadau muhimu na kutoa ushahidi utakaoonesha thamani ya hatua madhubuti katika kukabiliana na hatari zinazohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Meneja mwandamizi wa mpango wa kikanda wa Usimamizi wa Hatari ya Maafa katika Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa kilicho chini ya IGAD Ahmed Amdihun amesema, uzinduzi wa mradi huo unaashiria hatua muhimu katika juhudi za kikanda za kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha