

Lugha Nyingine
DRC yakataa mazungumzo yoyote na kundi la waasi la M23
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imekataa mazungumzo yoyote na kundi la waasi la M23.
Waziri wa ulinzi wa DRC Guy Kabombo amesema hayo jana alipohutubia vikosi vya jeshi, na kusema ameamuru mipango na maagizo yote kuhusu mazungumzo yanayodaiwa kufanywa na magaidi wa M23 yasitekelezwe.
Mapema siku hiyo, kundi la M23 lilitangaza kuwa liko tayari kufanya mazungumzo na serikali ya DRC baada ya kudai kuwa limechukua udhibiti wa Goma, mji muhimu mashariki mwa DRC.
Katika hotuba yake kwa taifa iliyotolewa jumatano wiki hii, rais wa DRC Felix Tshisekedi aliahidi kujibu vikali mashambulio ya kundi la M23, na kusema hatua zinaendelea kukomboa maeneo yote yanayoshikiliwa na kundi hilo nchini DRC.
Shughuli mbalimbali za kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China zafanyika katika Nchi Nyingi
Muonekano wa Kisiwa cha Weizhou katika Mkoa wa Guangxi, Kusini mwa China
Hafla ya Kukaribisha Panda wa China yafanyika katika Bustani ya Wanyama ya Adelaide, Australia
Shughuli mbalimbali zafanyika sehemu mbalimbali China kukaribisha Mwaka Mpya ujao wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma