Shambulizi baya zaidi la kufyatua risasi kwenye halaiki katika historia ya Sweden laua watu 10 shuleni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 05, 2025

Hii ni picha ya skrini iliyochukuliwa kutoka kwenye video ya mkutano na waandishi wa habari wa serikali ya Sweden uliofanyika jioni ya Februari 4, 2025. (Xinhua/ Zhu Haochen)

Hii ni picha ya skrini iliyochukuliwa kutoka kwenye video ya mkutano na waandishi wa habari wa serikali ya Sweden uliofanyika jioni ya Februari 4, 2025. (Xinhua/ Zhu Haochen)

HELSINKI - Shambulizi la kufytaua risasi shuleni katika mji wa katikati mwa Sweden wa Orebro ambalo polisi wamethibitisha Jumanne jioni kwamba limeua takriban watu kumi ni shambulizi baya zaidi la ufyatuaji risasi kwenye halaiki katika historia ya nchi hiyo, Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kristersson amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari jioni ya jana Jumanne.

Kwa mujibu wa jeshi la polisi, shambulizi hilo limetokea mchana katika Risbergska Skolan, ambacho ni kituo cha elimu, mjini Orebro ambapo mshukiwa wa ufyatuaji huo wa risasi ni miongoni mwa waliofariki.

Wakati uchunguzi na utafutaji zaidi ukiendelea, mamlaka zimesema idadi kamili ya waliofariki bado haijafahamika. Hata hivyo, taarifa za awali zinaonyesha kuwa mshukiwa ametekeleza shambulizi hilo peke yake, na polisi wameondoa ugaidi kuwa moja ya sababu.

Hii ni picha ya skrini iliyochukuliwa kutoka kwenye video ya mkutano na waandishi wa habari wa serikali ya Sweden uliofanyika jioni ya Februari 4, 2025. (Xinhua/ Zhu Haochen)

Hii ni picha ya skrini iliyochukuliwa kutoka kwenye video ya mkutano na waandishi wa habari wa serikali ya Sweden uliofanyika jioni ya Februari 4, 2025. (Xinhua/ Zhu Haochen)

Kristersson ametoa wito kwa umma kujiepusha na uvumi, akisisitiza kwamba mamlaka lazima zipewe nafasi kufanya uchunguzi wao.

"Umma wa Sweden unataka kujua sababu, lakini itabidi kusubiri majibu," amesema Waziri wa Sheria wa Sweden Gunnar Strommer kwenye mkutano na waandishi wa habari. "Kwa muda mwafaka, picha itakuwa dhahiri."

Mfalme Carl XVI Gustaf wa Sweden ametoa rambirambi katika taarifa yake, akiielezea siku hiyo kama "siku nyeusi" kwa Sweden. Ametoa pole kwa familia na marafiki wa waliofariki na majeruhi, na ameeleza shukrani kwa juhudi za polisi, waokoaji na wafanyakazi wa afya.

Picha iliyopigwa Septemba 24, 2023 ikionyesha doria ya polisi katikati mwa Stockholm, Sweden. (Xinhua/He Miao))

Picha iliyopigwa Septemba 24, 2023 ikionyesha doria ya polisi katikati mwa Stockholm, Sweden. (Xinhua/He Miao))

Risbergska Skolan hasa huhudumia watu wazima wenye umri wa zaidi ya miaka 20, huku pia kikitoa kozi za shule za msingi na sekondari na madarasa ya lugha ya Kiswidi kwa wahamiaji. Mji wa Orebro unapatikana umbali wa kilomita karibu 200 magharibi mwa Stockholm.

Akizungumza na Redio ya Sweden (SR), mtaalamu wa mambo ya usalama wa shule katika eneo hilo Lena Ljungdahl amesema kuwa ingawa vurugu za kutumia silaha shuleni zimekuwa nadra sana nchini Sweden, ghasia zimeongezeka nje ya taasisi za elimu, ikiwa ni pamoja na ufyatuaji risasi wa mara kadhaa karibu na shule katika miaka ya hivi karibuni.

"Nimekuwa nikitarajia hili. Shule si mahali palipotengwa. Kinachotokea nje kitatokea mapema au baadaye ndani ya shule," Ljungdahl amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha