

Lugha Nyingine
Utulivu warejeshwa mjini Goma nchini DRC, na hatari ya milipuko ya magonjwa yaongezeka
Picha hii iliyopigwa Februari 1, 2025 ikionyesha eneo la katikati mwa jiji la Goma, Jimbo la Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). (Picha na Zanem Nety Zaidi/Xinhua)
UMOJA WA MATAIFA - Wakati hali ya utulivu ikiwa imerejeshwa huko Goma, mji muhimu wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), hatari ya kuzuka kwa magonjwa, ikiwa ni pamoja na kipindupindu na Mpox, inaongezeka, maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema.
"Mjini Goma, kwa sasa, hali bado ni ya wasiwasi na tete, huku matukio ya kufyatua risasi ya hapa na pale yakiendelea, lakini ninaweza kusema kwamba kwa ujumla, utulivu umerejeshwa hatua kwa hatua," Naibu Katibu Mkuu wa Operesheni za Amani Jean-Pierre Lacroix amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika wiki iliyopita, Ijumaa.
"Maji na umeme vimerejeshwa katika sehemu kubwa ya mji, lakini tunaendelea kukabiliana na changamoto ya mabomu ambayo hayajalipuka ... kikwazo kikubwa sana kwa uhuru wa kutembea," amesema.
Njia za kutua na kupaa ndege kwenye uwanja wa ndege wa mji huo zimeharibiwa vibaya katika mapigano ya hivi karibuni na zimeshindwa kutumiwa. Misaada haiwezi kupelekwa kwa kuwa ni barabara pekee za kuingia za nchi jirani ya Rwanda ndizo zimefunguliwa, na njia za uchukuzi za ndani zimefungwa.
Lacroix amesema waasi wa kundi la M23 na Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) wanaendelea na usongaji wao mbele kwenda katika Mji wa Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini.
"Hiyo ni, bila shaka, suala lenye kutia wasiwasi," amesema.
Akikumbushia juu ya vitisho vilivyotolewa na maadui hao wa DRC kusonga mbele kuelekea mji mkuu wa Kinshasa, magharibi mwa nchi hiyo, Lacroix amesema, "Upotevu wa maisha na uharibifu vitakuwa vya kusikitisha sana."
Pia ameelezea hofu kwamba mgogoro huo sasa unaweza kupanuka.
Licha ya changamoto hiyo, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema wafanyakazi wa kutoa misaada wanachunguza uharibifu huo.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti serikali, mashirika ya ndani na ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu yameondoa maiti 700 katika mitaa ya Goma kati ya Jumapili na Alhamisi, na kwamba watu 2,800 wanaojeruhiwa walikuwa wakitibiwa.
Picha hii iliyopigwa Februari 1, 2025 ikionyesha wachuuzi wakiuza kuku kwenye soko la mtaani mjini Goma, Jimbo la Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). (Picha na Zanem Nety Zaidi/Xinhua)
Picha hii iliyopigwa Februari 1, 2025 ikionyesha wachuuzi wakiuza kuku kwenye soko la mtaani mjini Goma, Jimbo la Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). (Picha na Zanem Nety Zaidi/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma