

Lugha Nyingine
Ufugaji wa nyuki wapunguza ukataji wa miti katika eneo la kati la Tanzania
(CRI Online) Februari 05, 2025
Shirika la Mfuko wa Mazingira Duniani (WWF) tawi la Tanzania, limesema ufugaji wa nyuki katika Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora unasaidia kupunguza ukataji miti na kuhifadhi uwiano wa kipekee wa ikolojia mkoani humo.
Shirika hilo limesema katika taarifa yake kwamba ufugaji nyuki mkoani humo unahimiza uhifadhi wa misitu, kwani nyuki wanategemea vyanzo mbalimbali vya maua ili kupata chakula.
Mamia ya wakazi wa wilaya ya Sikonge wameacha uchomaji mkaa, uliokuwa unasababisha ukataji miti na uharibifu wa mazingira, na sasa wanajishughulisha na ufugaji wa nyuki, ambao ni muhimu katika kupunguza ukataji miti, hali ambayo inawaletea faida kubwa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma