Rais wa Kenya adhamiria kutokomeza ugaidi katika eneo la mpakani

(CRI Online) Februari 05, 2025

Rais William Ruto wa Kenya amedhamiria kuchukua hatua madhubuti kukomesha ukosefu wa usalama katika eneo la kaskazini mwa Kenya linalopakana na Somalia, ili kuzuia mashambulizi ya kuvuka mpaka yanayofanywa na kundi la Al-Shabaab.

Katika ziara yake ya siku nne kwenye eneo hilo, Rais Ruto amewaagiza maofisa waandamizi wa polisi kuongoza operesheni za usalama, ikiwemo juhudi za kuokoa maofisa watano wa serikali waliotekwa nyara na kundi la Al-Shabaab Jumapili.

Kamanda wa Polisi eneo la Mandera Kusini Julius Njeru amethibitisha mashambulizi ya Jumapili dhidi ya viongozi wa serikali ya mtaa, akisema maofisa hao walishambuliwa na kutekwa nyara wakati walipokuwa wakisafiri kikazi kutoka Wargadud kwenda Elwak.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, maofisa hao wamepelekwa nchini Somalia kwa kuwa eneo hilo liko karibu na mpaka kati ya Kenya na Somalia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha