

Lugha Nyingine
Kenya yatumia teknolojia ya China kuongeza viwango vya bidhaa na mauzo ya nje
(CRI Online) Februari 05, 2025
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Huduma ya Ithibati la Kenya (KENAS) Bw. Walter Ongeti, amesema Kenya inatumia teknolojia ya China kuongeza viwango vya bidhaa na mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi.
Bw.Walter Ongeti amesema KENAS imesaini mkataba wa maelewano na idara kama hiyo ya China ili kubadilishana maarifa kati ya nchi hizo mbili.
Bw. Ongeti amesema ushirikiano huo umeongeza uwezo wa maabara wa kukagua bidhaa zinazopelekwa kwenye soko la nje, na kwamba kupitia ushirikiano huo, mashirika ya uidhinishaji ubora wa bidhaa ya Kenya yametumia michakato na utaalamu unaolingana na viwango vya kimataifa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma