Miamala ya simu nchini Kenya yapungua kwa asilimia 17 mwaka 2024

(CRI Online) Februari 05, 2025

Benki Kuu ya Kenya CBK imesema, katika mwaka 2024 Wakenya walifanya miamala ya pesa kwenye simu za mkononi yenye thamani ya dola bilioni 51 za kimarekani, ikiwa ni punguo la asilimia 17 kutoka dola bilioni 61.5 za kimarekani mwaka juzi, ikidhihirisha kwamba wananchi wa nchi hiyo wanakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi.

Kwa mujibu wa benki hiyo, huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa miamala ya simu kupungua nchini humo. Mwaka 2023 wananchi wa Kenya walihamisha dola bilioni 61.5 za kimarekani ikiwa ni punguo kutoka dola bilioni 61.8 mwaka 2022, ambayo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa miamala kupungua katika miaka 17 iliyopita.

Benki hiyo imesema, mwaka jana kiasi cha juu zaidi cha pesa kilichohamishwa na wananchi kilikuwa dola bilioni 6.1 za kimarekani katika mwezi Februari, na kiasi cha chini zaidi kilikuwa dola bilioni 5.1 mwezi Septemba.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha