China yapinga vikali kauli za kutowajibika za Marekani juu ya suala la Mfereji wa Panama

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 06, 2025

BEIJING - Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian amesema Marekani hivi karibuni imetoa kauli za kutowajibika kuhusu suala la Mfereji wa Panama, na kupotosha, kushambulia na kuchafua kwa makusudi ushirikiano husika na kwamba China inapinga vikali na imetoa malalamiko kwa Marekani.

Akizungumza jana Jumatano wakati akijibu swali husika kwenye mkutano na waandishi wa habari, Lin ameongeza kuwa tangu Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) lilipotolewa mwaka 2013, maeneo ya ushirikiano na wigo wake umeendelea kupanuka na limekuwa jambo zuri maarufu la umma la kimataifa na jukwaa la ushirikiano wa kimataifa likiwa na ushiriki mkubwa.

Amesema, katika zaidi ya muongo mmoja uliopita kwa ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, pande mbalimbali zimeshikilia moyo wa Njia ya Hariri wa amani na ushirikiano, uwazi na ujumuishaji, kufunzana na kunufaishana, kufuata kanuni ya mashauriano ya kina na mchango wa pamoja kwa kunufaishana, kufanya kazi kwa matokeo yenye matunda katika ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kutoa mchango katika kuimarisha urafiki na kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii wa nchi husika, ambayo imepokelewa na nchi hizi, na watu wake.

"Kwa sasa, ushirikiano kati ya China na Panama chini ya pendekezo la BRI unafanyika kawaida na umepata matokeo yenye matunda," Lin ameongeza.

Amebainisha kuwa, China inatumai pande husika kuimarisha hali ya kujiamini, kupinga uingiliaji kutoka nje, na kufanya uamuzi sahihi huku ukitilia maanani kwa ujumla uhusiano wa pande mbili na maslahi ya muda mrefu ya watu wa nchi hizo mbili.

Wakati akijibu swali lingine kuhusu kampuni husika ya Hong Kong inayoendesha bandari karibu na Mfereji wa Panama, Lin amesema kuwa serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (SAR) tayari ilikuwa imetoa majibu.

Akibainisha kuwa Panama ni sehemu inayovutia uwekezaji mwingi wa kimataifa na imekuwa maarufu kwa utawala wake mzuri wa sheria na mazingira ya uwazi ya kibiashara, Lin amesema kuwa China inaamini kuwa itatoa mazingira ya haki na usawa kwa kampuni kutoka nchi na kanda zote, ikiwa ni pamoja na Hong Kong ya China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha