

Lugha Nyingine
Maofisa na viongozi wa kibiashara wakutana Kenya kuhimiza uhusiano wa kibiashara kati ya Afrika na Mashariki ya Kati
Viongozi wakuu wa serikali na wafanyabiashara wamekutana mjini Nairobi, wakiwa na matumaini ya kukuza uhusiano wa kibiashara kati ya Afrika na eneo la Mashariki ya Kati.
Mkutano huo wa siku mbili kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa baadaye, wenye kauli mbiu ya “Kuimarisha Maendeleo ya Kiuchumi na Uvumbuzi kati ya Afrika na Mashariki ya Kati” umewakutanisha wajumbe zaidi ya 200.
Naibu mkurugenzi wa masuala ya uchumi na kurugenzi ya biashara ya Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora ya Kenya Bw. Joseph Masila, amesema Afrika na eneo la Mashariki ya Kati zimefungamana siyo tu kwa historia bali pia kwa matarajio ya pamoja ya kiuchumi.
Ameongeza kuwa Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi (CEPA) uliosainiwa kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Kenya utawezesha biashara na kuongeza uwekezaji wa kigeni kwa biashara za maeneo yote mawili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma