

Lugha Nyingine
Maofisa wa nchi za Afrika waahidi uendelevu wa ufadhili wa kupambana na malaria licha ya sintofahamu toka kwa wahisani
Maofisa waandamizi wa nchi za Afrika wamesema ufadhili wa programu za kupambana na malaria katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara utaendelea, huku serikali zikihamasisha rasilimali za ndani na kuziba upungufu uliosababishwa na kukatishwa ghafla kwa uungwaji mkono kutoka kwa wahisani wa nchi za magharibi.
Kwenye mkutano wa siku moja ulioandaliwa na Baraza la Kutokomeza Malaria la Kenya na Muungano wa Viongozi wa kupambana na Malaria wa Afrika uliofanyika mjini Nairobi, maofisa hao wamejadili mikakati bunifu ya kuongeza ufadhili wa ndani ya Afrika wa programu za kupambana na malaria.
Dola za kimarekani takriban bilioni 6.3 zinahitajika kila mwaka ili kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria barani Afrika, na kulifanya bara la Afrika kuwa karibu kutokomeza ugonjwa huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma