Chama tawala nchini Tanzania chaadhimisha miaka 48 tangu kuanzishwa kwake

(CRI Online) Februari 06, 2025

Chama cha Mapinduzi (CCM), chama tawala nchini Tanzania, Jumatano kimeadhimisha miaka 48 tangu kuanzishwa kwake katika mji mkuu wa nchi hiyo, Dodoma, ambapo njiwa 500 wamerushwa angani ili kuonesha dhamira ya chama hicho katika kudumisha amani na utulivu nchini humo.

Akihutubia wanachama na wafuasi wa CCM waliojumuika katika Uwanja wa Jamhuri, mwenyekiti wa chama hicho katika mkoa wa Dodoma Bw. Adam Kimbisa, amemsifu mwenyekiti wa taifa wa CCM ambaye pia ni Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuchukua nafasi muhimu katika kuhimiza masikilizano na kuhakikisha utulivu nchini kote.

Akiongea katika maadhimisho hayo, Katibu Mkuu wa CCM Bw. Emmanuel Nchimbi amesisitiza ahadi ya chama hicho ya kufanya uchaguzi mkuu ulio huru na wa haki mwezi Oktoba mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha