Kenya yatangaza mpango mkakati wa kuwezesha watu wenye ulemavu

(CRI Online) Februari 06, 2025

Kenya imezindua mpango mkakati wa miaka mitano wa kuwezesha watu wenye ulemavu.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Umoja wa Watu Wenye Ulemavu wa Kenya (UDPK) Bibi Sally Nduta amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa mpango huo unatoa mwongozo kwa Kenya kutekeleza mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu, na ule wa Umoja wa Afrika kuhusu Haki za Watu Wenye Ulemavu.

Amesema, mpango huo utahakikisha watu wenye ulemavu nchini Kenya wanashinda changamoto kama vile upatikanaji mdogo wa huduma muhimu, na uwakilishi mdogo katika vyombo vya maamuzi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha