

Lugha Nyingine
China yasema inapinga kulazimisha watu wa Gaza kupoteza makazi yao
BEIJING - Gaza ni sehemu isiyoweza kutengwa ya ardhi ya Palestina, na China inapinga kulazimisha watu wa Gaza kupoteza makazi yao, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Guo Jiakun amesema jana Alhamisi kwenye mkutano na waandishi wa habari alipoulizwa kutoa maoni yake juu ya pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la "kuisafisha" na kuichukua Gaza.
Guo amesema kuwa Gaza inamilikiwa na watu wa Palestina na ni sehemu isiyotengeka ya eneo la Palestina, siyo chipu ya majadiliao ya michezo ya kisiasa, bado haiko kwa mawindo ya wenye nguvu.
Amesema, vita tayari vimeiacha Gaza katika uharibifu na mateso na kwamba jumuiya ya kimataifa, hasa nchi kubwa, zinapaswa kuungana mkono kuifanya Gaza kuwa bora zaidi, badala ya kuwa mbaya zaidi, kwa kutoa msaada wa kibinadamu na kusaidia katika ujenzi wake mpya.
"China inaunga mkono kithabiti haki halali za kitaifa za watu wa Palestina, inaamini kwamba 'Wapalestina kutawala Palestina' ni kanuni muhimu ambayo inapaswa kufuatwa katika utawala wa Gaza baada ya mgogoro, na inapinga kulazimisha watu wa Gaza kupoteza makazi yao," amesema.
Ameongeza kuwa, China inapenda kushirikiana na pande mbalimbali duniani kwa ajili ya utekelezaji wa suluhu ya nchi mbili kama njia ya msingi ya kusonga mbele, na kwa ajili ya suluhu ya kisiasa, ya mapema, ya haki kwa suala la Palestina, yaani, kuanzishwa kwa nchi huru ya Palestina ambayo ina mamlaka kamili kwa msingi wa mpaka wa mwaka 1967 huku Jerusalem Mashariki ikiwa mji wake mkuu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma