Kenya yapeleka walimu wa Kiswahili nchini Qatar

(CRI Online) Februari 07, 2025

Kenya imepeleka walimu wa lugha ya Kiswahili nchini Qatar, na kufanya idadi ya Wakenya katika eneo hilo la Ghuba kufikia 75,000.

Walimu hao wataungana na wauguzi na wafanyakazi wa usalama wanaojiandaa kufanya kazi nchini Qatar kwa sasa chini ya makubaliano ya wafanyakazi yaliyopo kati ya Nairobi na Doha.

Mkuu wa Mawaziri wa Kenya ambaye pia ni Waziri wa Diaspora na Masuala ya Kigeni Musalia Mudavadi alitoa tangazo hilo Jumanne alipompokea Balozi wa Qatar nchini Kenya Mohamed al-Enazi ofisini kwake.

Viongozi hao walijadili njia za kuongeza fursa kwa wafanyakazi wa Kenya nchini Qatar. Pia walijadili uwezekano wa Wakenya wenye ujuzi siyo tu kuboresha maisha yao bali pia kuchangia ukuaji wa uchumi wa Kenya kupitia utumaji pesa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha