Tanzania yazitaka halmashauri za wilaya kulinda umma dhidi ya mashambulizi ya wanyama pori

(CRI Online) Februari 07, 2025

Serikali ya Tanzania imesema halmashauri za wilaya zina wajibu wa kuweka utaratibu utakaolinda wananchi dhidi ya mashambulizi ya wanyama pori.

Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania Dk Pindi Chana amelieleza Bunge la Tanzania wajibu huo wa Halmashauri za Wilaya wakati akijibu kilio cha wabunge kuhusu jitihada zisizoridhisha za kudhibiti mashambulizi makali yanayosababishwa na wanyama pori kutoroka kwenye hifadhi.

Kwa mujibu wa waziri huyo, halmashauri za wilaya kwa kushauriana na Wizara ya Maliasili na Utalii, zinatakiwa kupanga mikakati ya kulinda wananchi dhidi ya mashambulizi hayo yanayofanywa na wanyama pori katika maeneo yao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha