

Lugha Nyingine
Reli ya Ethiopia-Djibouti yaongeza uwezo wa kusafirisha bidhaa
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Reli ya SGR ya Ethiopia-Djibouti (EDR) Bw. Takele Uma, amesema kampuni yake inapiga hatua kubwa kuongeza uwezo wa reli hiyo kusafirisha bidhaa zinazoagizwa kutoka nje na kuuzwa nje ya nchi.
Bw. Uma ameandika katika ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa X kuwa, kutokana na kuongezeka kwa vichwa vya treni na mabehewa, kampuni yake sasa inaweza kuhudumia maeneo mengi zaidi, ambayo yamepanuka kutoka Indode na Adama hadi Mojo, Dire Dawa na Sabata.
Tangu ilipozinduliwa mwaka 2018, reli hiyo iliyojengwa na China imeendelea kupanua soko na huduma zake za usafirishaji wa mizigo, ikiwemo huduma za ubora wa juu kama vile usafirishaji wa bidhaa za mnyororo baridi, treni za wanavijiji, na treni maalum za kusafirisha magari.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma