

Lugha Nyingine
Mashirika ya UN yatangaza vituo 15 vya uvumbuzi ili kuchochea mabadiliko ya kidijitali nchini Kenya
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yametangaza orodha ya vituo 15 vya uvumbuzi ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali nchini Kenya huku yakihimiza usawa na ujumuishaji.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa mjini Nairobi, na Mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Kenya, inasema mpango wa miaka mitatu wa Umoja wa Mataifa unaohusisha mfumo wa majukwaa ya kidigitali wa Kenya, unatarajiwa kuifanya Kenya kuwa kitovu cha uchumi wa maarifa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali ya Kenya Bw. John Tanui, amesema vituo hivyo vya ubunifu wa kidijitali vitatoa jukwaa la kukuza uvumbuzi, biashara na maendeleo endelevu.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema vituo hivyo vilivyoteuliwa vitatumika kama injini za uvumbuzi, mafunzo, na uwezeshaji wa jamii, na kuziba pengo la kidijitali nchini Kenya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma