Msemaji wa mpatanishi wa amani wa kikanda atoa wito wa mazungumzo ya kumaliza mgogoro mashariki mwa DRC

(CRI Online) Februari 07, 2025

Kanze Dena, msemaji wa ofisi ya rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyata ambayo pia ina jukumu la kuwa mpatanishi wa amani wa kikanda wa mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) amesema msukosuko wa kiusalama na kibinadamu unaoendelea mashariki mwa DRC unaweza kutatuliwa tu kwa njia ya mazungumzo.

Bi. Dena ambaye pia ni mwezeshaji wa Mchakato wa Nairobi unaoongozwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), amesema mchakato wa Luanda ulioanzishwa mwaka 2022 na kuidhinishwa na Umoja wa Afrika, na Mchakato wa Nairobi una uwezekano mkubwa zaidi wa utatuzi na kumaliza mgogoro wa mashariki mwa DRC.

Bi. Dena amesema ni kupitia uratibu wa karibu wa mazungumzo ya pande mbili kati ya Rwanda na DRC, na Mchakato wa Mazungumzo na Mikutano kuhusu Kongo, ndipo mgogoro unaoendelea unaweza kufikia hitimisho lenye matunda.

Amesema Rais wa zamani wa Kenyatta bado amedhamiria kutafuta njia za amani, kwa ushirikiano na DRC, washirika wa kikanda pamoja na wadau wa kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha