

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan wafanya dhifa ya kuwakaribisha wageni waheshimiwa wa kimataifa walioshiriki ufunguzi wa Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia
Mchana wa tarehe 7, Februari, rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba kwenye dhifa ya makaribisho. (Xie Huanchi/Xinhua)
Mchana wa tarehe 7, Februari huko Harbin, mkoani Heilongjian, rais Xi Jinping wa China na mkewe Peng Liyuan walifanya dhifa ya kuwakaribisha wageni waheshimiwa wa kimataifa walioshiriki kwenye ufunguzi wa Michezo ya tisa ya Majira ya Baridi ya Asia inayofanyika Harbin, Mkoa wa Heilongjiang wa China.
(Xie Huanchi/Xinhua)
Wageni hao waheshimiwa ni pamoja na Sultani wa Brunei Haji Hassanal Bolkiah Mu'izzaddin Waddaulah, rais Sadyr Japarov wa Kyrgyzstan, rais Asif Ali Zardari wa Pakistan, Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Korea Woo Won-shik, mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya kimataifa Thomas Bach, na naibu mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Olimpiki ya Asia Timothy Fok Tsun-ting.
Mchana wa tarehe 7, Februari, rais Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan wakipiga picha pamoja na wageni waheshimiwa. (Ding Haitao/Xinhua)
Mchana wa tarehe 7, Februari, watoto 40 wanaovaa mavazi ya kikabila wakiimba wimbo wa kienyeji wa Mkoa wa Heilongjiang wa China “Ngalawa kwenye Mto Wusuli”, kwa kuwakaribisha wageni waheshimiwa wa kimataifa. (Yan Yan/Xinhua)
Rais Xi akiwa kwa niaba ya serikali ya China na watu wa China alitoa hotuba kuwakaribisha kwa furaha wageni waheshimiwa wa kimataifa waliowasili China kushiriki kwenye ufunguzi wa Michezo ya tisa ya Majira ya Baridi ya Asia.
Xi alisema, idadi ya nchi na maeneo washiriki na idadi ya wachezaji wa michezo hiyo imeweka rekodi mpya katika historia ya Michezo ya Majira ya Baridi ya Asia. Anaamini chini ya juhudi za pamoja za Baraza la Olimpiki ya Asia na ujumbe wa kila nchi na kila eneo, michezo inayofanyika Mji wa Harbin itaonesha “sifa maalumu ya China, na mvuto murua mbalimbali wa Asia”.
Xi alisisitiza kuwa, michezo hiyo yenye kauli mbiu ya “Ndoto ya Pamoja ya Majira ya Baridi, Moyo Mmoja wa Asia”, inabeba matarajio na utafutaji wa pamoja wa watu wa Asia kwa amani, maendeleo na urafiki. Ni lazima kushikilia ndoto ya pamoja ya utulivu na msikilizano, ili kutoa nguvu ya Asia kwa ajili ya dunia yenye ncha nyingi iliyo na usawa na utaratibu.
Xi alisema, Harbin ni chimbuko la michezo ya kisasa ya majira ya baridi nchini China. Utamaduni na uchumi wa barafu na theluji hivi sasa ni msukumo mpya wa maendeleo ya sifa bora ya Harbin na kiunganishi kipya cha kufungua mlango kwa nje. Anawakaribisha watu kutembelea eneo hilo la ukarimu na uwazi, na kuwataka wachezaji kuwa wepesi kama nyoka walivyo katika mwaka mpya wa jadi wa nyoka wa China, na kujinyakua kijasiri mafanikio mazuri.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma