

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping asema China inapenda kushirikiana na IOC kuhimiza pamoja Michezo ya Olimpiki
Rais wa China Xi Jinping akikutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bach mjini Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Februari 7, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)
HARIBIN – Jana Ijumaa Rais wa China Xi Jinping amesema kuwa China inapenda kushirikiana na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kuendelea kusukuma mbele maendeleo ya Michezo ya Olimpiki.
Rais Xi alisema hayo alipokutana na Rais wa IOC Thomas Bach mjini Harbin, mji mkuu wa Mkoa wa Heilongjiang kaskazini mashariki mwa China ambaye yuko mjini humo kushiriki kwenye ufunguzi wa Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia.
Rais Xi ameeleza kuwa, China imeandaa kwa mafanikio mashindano makubwa ya michezo mbalimbali katika miaka ya hivi karibuni yaliyoonesha ushirikiano wa karibu kati ya China na IOC.
Rais Xi amesema, China inaendeleza kwa nguvu sekta yake ya michezo na kusonga mbele kuelekea kwenye lengo la kujenga China yenye nguvu ya michezo na watu wenye afya, ambayo itatoa mchango mpya siku hadi siku kwa maendeleo ya michezo ya kimataifa.
Kwa upande wake Bach ameipongeza China kwa kutetea na kutekeleza dhana ya mshikamano na ushirikiano, usawa na heshima, kushikilia ushirikiano wa pande nyingi, kupinga kuingiza siasa kwenye michezo, na kuunga mkono ushiriki mpana wa nchi zinazoendelea katika michezo ya kimataifa.
Ameeleza imani yake kuwa China itaendelea kupata mafanikio makubwa na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya amani na maendeleo ya Dunia, na mambo ya maendeleo ya binadamu.
Viongozi waandamizi wa China akiwemo Cai Qi walihudhuria mkutano huo.
Rais wa China Xi Jinping akikutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bach mjini Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Februari 7, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma