Rais wa Slovenia akosoa vikwazo vya Marekani dhidi ya ICC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 08, 2025

Picha hii iliyochukuliwa kutoka kwenye tovuti rasmi ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ikionyesha kichwa cha taarifa iliyotolewa Februari 7, 2025, ambapo Mahakama hiyo inalaani vikwazo vya Marekani dhidi yake.

LJUBLJANA - Rais Natasa Pirc Musar wa Slovenia amesema kwamba vikwazo vya Marekani dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) vinadhoofisha msingi wa sheria ya kimataifa ya uhalifu.

"Vikwazo hivi vinawakilisha kutojali waziwazi utekelezaji wa sheria kama msingi wa uhusiano wa kisasa wa kimataifa," Musar amesema katika taarifa yake iliyotolewa jana Ijumaa.

Ameeleza uungaji mkono kwa pendekezo lililotolewa na Nchi Watia Saini kwenye Mkataba wa Roma ili kulinda uhuru wa shirika hilo la kimataifa lenye makao yake makuu The Hague na wafanyakazi wake.

"Marekani inatuma ujumbe wenye hatari: kwamba majaji wa ICC wataadhibiwa kwa kufuata tu haki dhidi ya wale wanaoshukiwa kufanya uhalifu mkubwa," amesema, akiongeza kuwa hakikisho pekee ambalo watu binafsi wanapaswa kuwa nalo dhidi ya mashtaka ni kwamba "hawashiriki katika uhalifu wa kutisha dhidi ya binadamu."

Wizara ya Mambo ya Nje na Mambo ya Ulaya ya Slovenia imesema siku hiyo hiyo ya Ijumaa kwamba taasisi za mahakama zinapaswa kulindwa dhidi ya vitisho.

Rais Donald Trump wa Marekani akimkaribisha Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya Marekani White House mjini Washington D.C., Marekani, Februari 4, 2025. Trump alikutana na Netanyahu mjini humo siku ya Jumanne wiki hii. (Xinhua/Hu Yousong)

Siku ya Alhamisi wiki hii, Rais wa Marekani Donald Trump alitia saini amri ya kuiwekea vikwazo ICC, akidai kuwa mahakama hiyo imejihusisha na "vitendo haramu na visivyo na msingi" vinavyoilenga Marekani na mshirika wake wa karibu Israel.

Novemba 21, 2024, ICC ilitoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Yoav Gallant, ikirejelea tuhuma za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu waliofanya katika operesheni ya kijeshi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza. Hati zake hizo za kukamatwa pia zilijumuisha kamanda wa Hamas Mohammed Deif wakati huo.

Slovenia ililitambua Taifa la Palestina mwezi Juni mwaka jana na inaendelea kuunga mkono suluhu ya nchi mbili katika mgogoro kati ya Israel na Hamas.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha