

Lugha Nyingine
Majimbo mawili nchini Sudan yatajwa kuwa hatarini kutokana na kuongezeka kwa mapigano
Naibu Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema, mapigano ya hivi karibuni yamefanya majimbo mawili ya Kordofan Kusini na Blue Nile nchini Sudan kuwa hatarini zaidi.
Akizungumza na wanahabari Alhamisi, Haq amesema idadi ya vifo vya raia kutokana na mashambulio ya makombora hivi karibuni katika mji mkuu wa Jimbo la Kordofan Kusini, Kadugli, imefikia 80 huku wengine wengi wakiwa wamejeruhiwa.
Kwa mujibu wa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa anayeratibu masuala ya kibinadamu nchini Sudan, Clementine Nkweta-Salami, mapigano yanaendelea kuongezeka kwa kasi kubwa, na amelaani vikali matumizi ya wanawake na watoto kama kinga ya kimwili katika mji wa Kadugli, kuzuiwa kwa misaada ya kibinadamu, na kushikiliwa kwa raia, wakiwemo watoto.
Bi. Nkweta-Salami ametoa wito kwa pande zote zinazopigana nchini Sudan kupunguza kuongezeka kwa vita, kulinda raia na miundombinu ya kiraia, na kuruhusu mashirika ya kibinadamu kufikisha misaada kwa usalama kwa wale wanaohitaji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma