Malawi kuondoa Jeshi lake DRC

(CRI Online) Februari 08, 2025

Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, amemuagiza Kamanda wa Jeshi la nchi hiyo kujiandaa kuondoa majeshi ya Malawi kutoka eneo la mashariki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Taarifa iliyotolewa na serikali ya nchi hiyo imesema, uamuzi wa Rais Chakwera unalenga kuheshimu tangazo la kusimamishwa mapigano kati ya pande hasimu lilitolewa na waasi wa M23, ambao walifanya mashambulizi katika mji wa Nyabibwe, Jimbo la Kivu Kusini, DRC.

Kuondolewa kwa wanajeshi wa Malawi kutatoa fursa ya kuendeleza mazungumzo ya kuelekea amani ya kudumu.

Rais Chakwera amekumbana na shinikizo kubwa la kimataifa kuhusu uamuzi wa kuondoa majeshi ya Malawi Mashariki mwa DRC, hasa baada ya wanajeshi watatu wa Malawi kuuawa katika mashambulizi ya M23 mjini Goma.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha