Serikali ya Tanzania yathibitisha kusitishwa misaada ya Marekani

(CRI Online) Februari 08, 2025

Waziri Mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa ameeleza msimamo wa Serikali ya Tanzania kuhusu mabadiliko ya sera za misaada ya Marekani chini ya utawala wa Rais Donald Trump, akisisitiza kuwa Tanzania inatakiwa kujikita katika kujitegemea kiuchumi.

Akijibu maswali ya wabunge kwenye mkutano wa bunge la Tanzania unaoendelea katika mji mkuu wa nchi hiyo Dodoma, Bw. Majaliwa amesema serikali ya Marekani imesitisha baadhi ya misaada kwa Tanzania na nchi nyingine zinazoendelea kupitia Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

Amesema mabadiliko hayo ni sehemu ya sera mpya za mambo ya nje za Marekani, ambazo zinaweza kuwa na athari kwa baadhi ya sekta nchini Tanzania, akisisitiza kuwa Tanzania imejipanga kuhakikisha uchumi wake unajitegemea ili kuepuka utegemezi wa misaada kutoka nje.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha