

Lugha Nyingine
Raia 25 wauawa katika shambulizi linaloshukiwa kuwa la kigaidi kaskazini mwa Mali
Jeshi la Mali limesema raia takriban 25 wameuawa na wengine 13 kujeruhiwa katika shambulizi linaloshukiwa kuwa la kigaidi lilitokea Ijumaa kaskazini mwa Mali.
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumamosi, jeshi hilo limesema kuwa, kundi la kigaidi linalojumuisha watu wengi wenye silaha lilivizia msafara uliokuwa ukisindikiza raia karibu na mji wa Gao wa kaskazini mwa Mali.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa, wengi wa waliouawa ni wachimba madini migodini wa kigeni waliokuwa wakielekea kwenye mgodi wa dhahabu huko Gao.
Katika taarifa hiyo, jeshi limesema kwamba, magari matatu ya kiraia yalishambuliwa katika shambulizi hilo na hadi kufikia siku hiyo ya Jumamosi wakati taarifa inatoka, miili 19 ya watu wenye silaha ilikuwa imepatikana, na wanamgambo wanne walikuwa wamekamatwa.
Imeeleza kuwa, hakuna kundi au mtu binafsi aliyedai kuhusika na shambulizi hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma