

Lugha Nyingine
“Matembezi ya urafiki” kati ya China na Burundi yafanyika Bujumbura
Matembezi ya urafiki kati ya China na Burundi yaliyoongozwa na Ubalozi wa China na Jumuiya ya Urafiki kati ya Burundi na China (ASIBU) yamefanyika Jumamosi mjini Bujumbura.
Balozi wa China nchini Burundi Bi. Zhao Jiangping, Mwenyekiti wa ASIBU Bw. Ferdinand Nderagakura, mkurugenzi wa uhusiano wa pande mbili katika wizara ya mambo ya nje ya Burundi Bw. Ernest Niyokindi, na maofisa wengine wa Burundi na wachina wanaoishi na kufanya kazi nchini Burundi wameshiriki katika matembezi hayo.
Matembezi hayo ya takriban kilomita tano yamefanyika kupitia barabara ya Mao, iliyopewa jina la kiongozi wa zamani wa China Mwenyekiti Mao Zedong, na kwenye Shule ya Kitaaluma ya Kigobe, iliyojengwa kwa uungwaji mkono wa China.
Balozi wa China nchini Burundi Bi. Zhao Jiangping amesema kwenye shughuli hiyo kuwa anatumai mashirika ya urafiki yasiyo ya kiserikali ya China na Burundi yatatekeleza kikamilifu jukumu la kuimarisha mabadilishano kati ya watu wa pande mbili na kusaidia kuendeleza ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma