IGAD yateua mwenyekiti mpya katika kusimamia amani ya Sudan

(CRI Online) Februari 10, 2025

Shirika la usimamizi wa amani la Sudan limesema, Shirika la Maendeleo la Serikali za Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) limeidhinisha uteuzi wa George Aggrey Owinow kutoka Kenya kuwa mwenyekiti mpya wa Kamati Mpya ya Pamoja Iliyoundwa Upya ya Usimamizi na Tathmini (RJMEC).

Taarifa iliyotolewa na RJMEC mjini Juba mwishoni mwa wiki imesema meja jenerali mstaafu Owinow ameteuliwa na serikali ya Kenya na kuidhinishwa na IGAD, kuchukua nafasi ya Charles Tai Gituai aliyekuwa kwenye wadhifa huo tangu mwezi Agosti mwaka 2020.

Taarifa hiyo imesema wakati huu ni kipindi muhimu cha kuingiza tena nguvu kwenye makubaliano ya amani, na kazi muhimu mfululizo zinapaswa kutekelezwa, ili kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya uchaguzi utakaofanyika mwezi Desemba mwaka 2026.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha