Je, uwekezaji wa nchi za nje zaondoka China kwa wingi? (Swali la Wasomaji)

By Luo Shanshan (People’s Daily) (Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 10, 2025

Msomaji wa Tovuti ya Gazeti la Umma (People’s Daily Online) anauliza: Kuna vyombo vya habari vya mtu binafsi mtandaoni vinavyosema “uwekezaji wa nchi za nje unaondoka China kwa wingi.” Je, hali hii ni kweli? Nimetafuta kwenye mtandao wa Intaneti nikagundua kwamba mnamo mwaka 2024, matumizi ya mitaji ya kigeni ya China yalipungua kwa 27.1% kuliko mwaka 2023, huku kampuni mpya za nchi za nje zilizoanzishwa nchini China zimeongezeka kwa 9.9% kuliko mwaka 2023. Je, takwimu hizo siyo zinapingana?

Jibu: Msomaji huyu ameangalia kwa makini sana. Ili kujibu swali hilo, nataka kuanzia jambo lililotokea karibu nasi.

Sote tunajua kuhusu maduka makubwa ya Walmart. Je, unaona hivi karibuni maduka mengi ya Walmart yamefungwa? Umeona mara kwa mara habari kuhusu “Walmart kuondoka China”?

Lakini huo ndio ukweli wa mambo yote? Siyo habari ya hakika !

Mnamo Desemba 18, 2024, maduka ya uwanachama ya Sam ambayo ni tawi la Walmart yalifungua duka lake la 52 nchini China. Inadhihirika zaidi kuwa katika robo ya tatu ya mwaka 2024, uuzaji wa Walmart nchini China umeongezeka kwa 17%.

Habari zinasemekana mara kwa mara Kampuni hiyo “itaondoka China”, lakini inadumu ongezeko la uuzaji wake katika soko la China. Je, mambo hayo yanapingana?

Hali hii inaonesha mabadiliko ya soko la China: Kutokana na mwelekeo wa mahitaji ya wateja ya kibinafsi zaidi na ya aina nyingi zaidi, na kuongezeka kwa kampuni za mauzo ya rejareja za China, mtindo wa biashara ya jadi umeachwa na watu wengi nchini China, na kampuni za nchi za nje lazima zifuate kwa kasi mabadiliko ya soko la China ili kupata mafanikio.

Kwa ufupi, zama tulizonazo zinaendelea, hali ya soko la China imebadilika na kuwa tofauti na zamani, ambapo uhusiano kati ya China na uwekezaji wa nchi za nje pia umekuwa na mabadiliko mapya.

Katika miaka ya hivi karibuni, China imechukua hatua nyingi zaidi za kufungua mlango kwenye kiwango cha juu zaidi, ambazo zimepunguza matakwa ya kuingia soko la China kwa uwekezaji wa nchi za nje. Kampuni nyingi zaidi za nchi za nje zenye ukubwa wa kati au mdogo zimeingia soko la China, hali ambayo ni sababu muhimu ya kuongezeka haraka kwa idadi ya kampuni mpya za nchi za nje zilizoanzishwa nchini China.

Na kwa nini ukubwa wa kuingiza uwekezaji wa nchi za nje umepungua?

Tokea mwaka 2021, ukubwa wa kuingiza uwekezaji wa nchi za nje ulikuwa wa zaidi ya Yuan trilioni 1 (sawa na dola za kimarekani bilioni 136.85 kwa uwiano wa hivi sasa) kwa miaka mitatu mfululizo, ambapo mitaji ya kigeni imeingia kwa kiasi kikubwa na kukidhi mahitaji ya pamoja. Kwa hivyo ni hali ya kawaida kwa ukubwa huo uliopungua mwaka 2024.

Kutupia macho hali ya muda mrefu baadaye, uwekezaji wa kimataifa duniani unaelekea zaidi sekta ya huduma na unazidi kuwa wa mitaji michache, kwa hivyo hali isiyolingana kati ya matumizi ya mitaji ya kigeni na idadi ya kampuni mpya itatokea katika kipindi kipindi.

Hakuna shaka kwamba, China ikiwa nchi inayodumisha maendeleo yenye msukumo mkubwa ni “keki tamu” machoni mwa wawekezaji wa nchi za nje, lakini katika nchi ya China yenye ushindani wa kutosha na soko la uwazi, kampuni za nchi za nje lazima zifanye juhudi kubwa ili kukita mizizi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha