Mkuu wa IMF aona maendeleo makubwa yamepatikana katika mageuzi ya uchumi ya Ethiopia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 11, 2025

Picha hii iliyopigwa Februari 13, 2024, ikionyesha mwonekano wa jiji la Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Li Yahui)

Picha hii iliyopigwa Februari 13, 2024, ikionyesha mwonekano wa jiji la Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Li Yahui)

ADDIS ABABA - Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kristalina Georgieva amesifu maendeleo makubwa yaliyopatikana nchini Ethiopia katika mpango wake wa mageuzi ya kiuchumi yaliyoanzishwa nchini humo.

Georgieva, ambaye aliwasili Jumamosi mjini Addis Ababa katika ziara rasmi ya siku mbili, amekutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Waziri wa Fedha Ahmed Shide, gavana wa Benki ya Taifa ya Ethiopia Mamo Mihretu, na Waziri wa Mipango na Maendeleo Fitsum Assefa, na maofisa wengine waandamizi wa Ethiopia.

"Imekuwa vizuri sana kukutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia kujadili ufanisi mzuri wa uchumi wa Ethiopia," amesema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii. "Nimeona hapa Addis Ababa dalili za uchumi wa soko wenye kustawi unaoongozwa na sekta binafsi, na nina furaha kwamba IMF ni mshirika wa ajenda ya serikali ya mageuzi hayo."

Baada ya kukutana na Georgieva, Abiy amesema mpango wa mageuzi ya uchumi mkuu wa Ethiopia, ambao unaungwa mkono na moja ya mipango mikubwa zaidi ya ufadhili ya IMF, mpango huo unatokana na matarajio ya nchi hiyo na ajenda ya mageuzi iliyoanzishwa nchini humo ambayo inaeleza wazi matarajio ya ukuaji na maendeleo ya nchi hiyo.

"Tunathamini uungaji mkono wa kiufundi na kifedha wa IMF wa kila mara, vilevile juhudi na mchango wako binafsi (Georgieva) katika mpango wetu wa mageuzi ya uchumi," Abiy amesema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii. "Tumechukua hatua madhubuti, za kina na za kihistoria ili kuzishinda changamoto za muda mrefu za uchumi mkuu."

Picha hii iliyopigwa Februari 13, 2024, ikionyesha mwonekano wa jiji la Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Li Yahui)

Picha hii iliyopigwa Februari 13, 2024, ikionyesha mwonekano wa jiji la Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Li Yahui)

Wizara ya Fedha ya Ethiopia imesema, mikutano hiyo ya ngazi ya juu inafuatilia zaidi mageuzi ya uchumi yanayoendelea nchini humo, uungaji mkono unaotolewa na IMF, na matarajio ya kuendelea kwa ushirikiano ili kuhimiza utekelezaji wa ajenda ya uchumi ya nchi hiyo.

Mkuu huyo wa IMF pia alitembelea kituo cha mipango ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kituo cha ujengaji upya wa kimwili wa wanawake na shule ya bweni ya watu wenye ulemavu wa kuona mjini Addis Ababa. Amesema mipango kama hiyo "inaonyesha namna gani matumizi lengwa mazuri ya kijamii yanaweza kuleta fursa na kubadilisha maisha."

Mageuzi hayo ya Kiuchumi yaliyoanzishwa Nchini ni mwongozo wa mageuzi ya kiuchumi ya Ethiopia unaolenga kuifanya nchi hiyo kuwa "Alama ya Ustawi wa Afrika ifikapo mwaka 2030."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha