

Lugha Nyingine
Kenya yaapa kutanguliza ushirikiano na usalama wa kikanda na washirika wa kimataifa
Rais wa Kenya William Ruto amesema serikali yake itaendelea kuweka kipaumbele katika mafungamano ya kikanda, uhusiano wa ndani ya Afrika, diplomasia ya kiuchumi na amani na usalama duniani huku ikitafuta maeneo mapya ya ushirikiano na washirika wa kimataifa.
Rais Ruto amesema hayo jana Jumatatu mjini Nairobi, katika hotuba yake ya kila mwaka kwa wakuu wa tume za kulinda amani na mashirika ya kimataifa.
Ameeleza kuwa Kenya ambayo imekuwa ikiongoza mipango ya amani katika Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika, bado ni mshirika mwenye dhamira katika kuhakikisha amani na usalama wa kikanda na kimataifa.
Ruto amesisitiza tena kuwa amani na usalama vinasalia kuwa msingi wa dira ya Kenya ya kuwa eneo lenye ustawi na utulivu akisema kuwa, lengo kuu ni kuunda ushirikiano unaoleta manufaa halisi kwa watu wa Kenya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma