

Lugha Nyingine
Rwanda yazidisha kampeni ya kupambana na rushwa katika mahakama
Rwanda imezindua kampeni kali ya kupambana na rushwa katika mahakama, huku Jaji Mkuu wa nchi hiyo Domitilla Mukantaganzwa akibainisha hatua za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi ya watumishi wa mahakama waliohusika na ufisadi.
Akizungumza katika uzinduzi wa Wiki ya Kupambana na Ufisadi siku ya Jumatatu mjini Kigali, Mukantaganzwa amesema kuwa rushwa bado ni kikwazo kikubwa katika utoaji haki wa sheria.
Amesema, kati ya mwaka 2020 na 2024, mahakama nchini humo iliadhibu majaji, makarani wa mahakama na wafanyakazi wengine wa mahakama kwa ufisadi, ambapo makarani wawili wa mahakama na hakimu mmoja walifungwa.
Jaji Mukantaganzwa ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya rushwa kwa kutoa taarifa kuhusu majaribio ya rushwa na kutoa mrejesho wa huduma za mahakama. Amesema utoaji huduma duni, mara nyingi huweka mazingira ya rushwa kustawi.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Rushwa ya Rwanda 2024 iliyotolewa na “Transparency International Rwanda”, kiwango cha rushwa nchini humo kilishuka hadi asilimia 18.5 mwaka 2024 kutoka asilimia 22 mwaka 2023.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma