Pembe ya Afrika kupata dola za Kimarekani zaidi ya milioni 4 katika kushughulikia tatizo la njaa

(CRI Online) Februari 11, 2025

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema Umoja wa Ulaya umetoa dola milioni 4.13 za kimarekani kuunga mkono mradi wa pamoja wa kulinda watu wanaoishi katika mazingira magumu katika Pembe ya Afrika kutoka kwenye athari za hali mbaya za mabadiliko ya tabianchi, migogoro na watu kupoteza makazi.

Shirika hilo limesema katika taarifa yake siku ya Jumatatu kwamba, mpango huo utaunga mkono watu laki 4.5 walioko katika mazingira magumu nchini Ethiopia na Somalia ndani ya miaka miwili kwa kupunguza athari za mishtuko tabiriwa ya tabianchi kabla haijawa majanga kupitia kuimarisha uwezo wa mashirika ya hali ya hewa katika kutoa utabiri sahihi na kwa wakati, kuwezesha mwitikio bora zaidi wa jamii na serikali.

“Kuongezeka kwa hali mbaya za mabadiliko ya tabianchi kama vile ukame na mafuriko kunazidisha visababishi vilivyopo vya njaa kama vile mapigano, watu kuhama makazi yao na uchumi kuyumba” Naibu Mkurugenzi wa WFP anayeshughulikia mambo ya Afrika Mashariki Rukia Yacoub amesema katika taarifa yake iliyotolewa mjini Nairobi nchini Kenya.

Amesema, hatua za mapema zinaweza kuokoa maisha, kuimarisha uwezo wa watu katika kukabiliana na changamoto za mbele, na kupunguza shinikizo la rasilimali zisizotosheleza za mashirika ya misaada ya kibinadamu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha