

Lugha Nyingine
Mpendekezaji wa Sehemu Bora za Kutalii katika Majira Mazuri: Mwanzo wa Majira ya Mchipuko—Siku ya Lichun
Habari, Hamjambo, mimi ni Sisi mpenda safiri! Siku ya Lichun ni Mwanzo wa Majira ya Mchipuko, kipindi cha kwanza cha vipindi 24 vya hali ya hewa katika kalenda ya jadi ya kilimo ya China. Fuata nami na kutumia safari hii kubaini uzuri wa misimu minne!
Tumefika!
Ili kuhisi kuwadia kwa majira ya mchipuko, nimefika katika Mji wa Quzhou, Mkoa wa Zhejiang, mji maarufu wa kihistoria na kitamaduni wa China. Hapa, hali ya hewa ni ya uvuguvugu katika majira ya mapema ya mchipuko, na mambo yote yameanza kufufuka, yakileta hamasa na nguvu ya majira ya mchipuko.
Siku ya Lichun inawakilisha mwanzo wa majira ya mchipuko na mwanzo wa misimu minne ya mwaka. Katika zama za kale, Mwanzo wa Majira ya Mchipuko yaligawanywa katika vipindi vitatu: kipindi cha kwanza ni upepo wa mashariki unaleta joto na kuyeyusha barafu; kipindi cha pili ni wadudu kuamka katika hali ya kaputi; kipindi cha tatu ni samaki kuogelea kwenye mto ulioyeyuka.
"Majira ya Mchipuko yamewadia!"
Katika zama za kale, katika siku ya Lichun, watu walikuwa wakibandika Chunlian(karatasi zinazoandika maneno ya baraka), kuning'iniza mabango ya majira ya mchipuko, na kubandika michoro ya majira ya mchipuko ili kukaribisha majira ya mchipuko. Desturi ya kuvutia zaidi ni kumpiga mjeledi “Ng’ombe” aliyetengenezwa kwa karatasi, kuomba mavuno mazuri na hali nzuri ya hewa katika mwaka mpya.
Katika siku ya Lichun, watu pia wana mila ya "kung’ata majira ya mchipuko". "Kung’ata Majira ya Mchipuko" kunamaanisha kula panikeki na chapati. Unapong’ata na kula kipande kidogo, utahisi ladha ya majira ya mchipuko!
"Katika siku ya Lichun, hali ya hewa imekuwa joto kidogo, na barafu zimeanza kuyeyuka. Majira ya mchipuko yanapowadia, mimea na miti hujua." Majira ya mchipuko yanakuja. Ninawatakia kila la heri ya majira ya mchipuko marafiki zangu walio mbali. Natumai kila mmoja anaweza kuhisi uhai na matumaini ya majira ya mchipuko!
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma