China inapenda kuhimiza maendeleo ya AI na nchi nyingine: Naibu Waziri Mkuu wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 12, 2025

Mjumbe Maalum wa Rais Xi Jinping wa China Zhang Guoqing, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na naibu waziri mkuu wa Baraza la Serikali la China, akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa nchi na serikali na wawakilishi wa ngazi ya juu kutoka nchi zaidi ya 30, pamoja na viongozi wa mashirika ya kimataifa, baada ya Mkutano wa Kilele kuhusu Hatua za AI mjini Paris, Ufaransa, Februari 11, 2025. (Xinhua/Gao Jing)

PARIS - Mwakilishi Maalum wa Rais Xi Jinping wa China Zhang Guoqing amesema China inapenda kushirikiana na nchi nyingine kuhimiza maendeleo, kulinda usalama, kunufaisha mafanikio katika nyanja ya akili mnemba (AI), na kujenga kwa pamoja jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.

Zhang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na naibu waziri mkuu wa Baraza la Serikali la China ametoa kauli hiyo katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Kilele kuhusu Hatua za AI, ambao umefanyika mjini Paris, Ufaransa kuanzia Februari 10 hadi 11.

Wajumbe wakihudhuria kikao cha wadau wote kwenye Mkutano wa Kilele kuhusu Hatua za AI mjini Paris, Ufaransa, Februari 11, 2025. (Xinhua/Gao Jing)

Wajumbe wakihudhuria kikao cha wadau wote kwenye Mkutano wa Kilele kuhusu Hatua za AI mjini Paris, Ufaransa, Februari 11, 2025. (Xinhua/Gao Jing)

AI imekuwa nguvu muhimu katika duru mpya ya mapinduzi ya kisayansi na kiteknolojia na mageuzi ya kiviwanda, Zhang amesema, akisisitiza kuwa China kila mara imekuwa ikishiriki katika ushirikiano wa kimataifa na usimamizi juu ya AI kwa mtazamo wa kuwajibika sana.

“Oktoba 2023, Rais Xi Jinping alianzisha Pendekezo la Dunia la Usimamizi wa AI, ambalo lilipendekeza suluhu ya China na kutoa mchango wa hekima ya China kwa maendeleo na usimamizi wa AI,” Zhang amebainisha.

Katika kukabiliana na fursa na changamoto zinazoletwa na maendeleo ya AI, Zhang ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutetea kwa pamoja kanuni ya kuendeleza AI kwa mambo mema, kuzidisha ushirikiano wa kibunifu, kuimarisha ujumuishaji na manufaa, na kuboresha usimamizi wa kimataifa.

Pia amealika jumuiya za wabunifu wa programu kutoka duniani kote kushiriki katika Mkutano ujao wa Dunia wa Wabunifu programu Mwaka 2025, uliopangwa kufanyika kuanzia Februari 21 hadi 23 mjini Shanghai, China.

Kwenye mkutano huo mjini Paris, wakuu wa nchi na serikali na wawakilishi wa ngazi ya juu kutoka nchi zaidi ya 30, pamoja na viongozi wa mashirika ya kimataifa, kwa pamoja wametia saini Taarifa juu ya Akili Mnemba iliyo Jumuishi na Endelevu kwa Watu na Sayari ya Dunia.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akikutana na Mjumbe Maalum wa Rais Xi Jinping wa China Zhang Guoqing, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na naibu waziri mkuu wa Baraza la Serikali la China, mjini Paris, Ufaransa, Februari 11, 2025. (Xinhua/Gao Jing)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha