

Lugha Nyingine
China yapokea Airbus A350 ya kwanza ambayo haijapakwa rangi kwa kufanya kazi ya kukamilisha na kuikabidhi kwa mteja
Ndege ya Airbus A350 ambayo haijapakwa rangi na kukamilishwa ikionekana huko Tianjin, kaskazini mwa China, Februari 11, 2025. (Xinhua)
TIANJIN - Ndege aina ya Airbus A350 ambayo haijapakwa rangi na kukamilishwa imeruka kutoka Toulouse, Ufaransa, hadi Mji wa Tianjin kaskazini mwa China siku ya Jumanne, hii ni mara ya kwanza kwa ndege ya aina hiyo kuwasili Tianjian katika mwaka 2025, kampuni ya kuunda ndege ya Ulaya, Airbus imesema.
Ndege hiyo, ambayo imekamilisha uundaji wake nje ya China, itafanyiwa ufungaji vifaa wa mwisho wa sehemu ya kukaa abiria, kupakwa rangi, na kufanya majaribio ya usafiri wa ndege katika Kituo cha Kukamilisha Kazi cha Airbus Tianjin Widebody (C&DC) kabla ya kukabidhiwa kwa mteja rasmi.
Kampuni hiyo ya Airbus ilianzisha Mstari wake wa Mwisho wa Kuunganisha Sehemu za Ndege za aina ya A320 mjini Tianjin mwaka 2008, ikiwa ni kiwanda chake cha kwanza cha uzalishaji nje ya Ulaya. C&DC, kituo cha C&DC kilianzishwa mwaka 2017, huu ni mradi wa kwanza wa aina yake nje ya Ulaya, ulianza uungaji mkono wa kukamilisha uundaji wa ndege ya aina A350 na kukabidhi kwa wateja mwaka 2020.
Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2024, kituo cha C&DC kilikuwa kimekabidhi kwa wateja ndege 767 za aina ya A320, ndege 16 za A330 na 25 za A350.
"China ni soko kubwa la Airbus la nchi moja duniani," amesema George Xu, naibu mtendaji mkuu wa Airbus ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airbus Tawi la China.
Xu ameeleza kuwa, ndege zilizokabidhiwa kwa wateja wa China zinachukua asilimia takriban 20 ya ndege zote za Airbus zilizokabidhiwa kwa wateja duniani kote kwa mwaka. Amesema, hivi sasa nafasi ya kampuni hiyo kwenye soko la China imechukua asilimia zaidi ya 50 kutoka asiliia 20 ya mwaka 2008.
Xu amesema mwaka 2025 ni maadhimisho ya miaka 40 tangu ndege za abiria za Airbus kuingia soko la China Bara, na kwamba kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na washirika wa anga wa China ili kusukuma mbele maendeleo ya sifa bora ya sekta ya usafiri wa ndege ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma