

Lugha Nyingine
Botswana inayotegemea almasi yalenga kuendeleza uchumi mbalimbali
Ndaba Gaolathe (katikati), makamu rais wa Botswana ambaye pia ni waziri wa fedha wa nchi hiyo, akiwasilisha bajeti ya kwanza ya Bunge la 13 huko Gaborone, Botswana, Februari 10, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)
GABORONE - Makamu rais wa Botswana Ndaba Gaolathe amesema Jumatatu kuwa, shughuli za uchimbaji almasi nchini humo zimekabiliwa na mustakabali usio na uhakika, Botswana inatafuta kuendeleza kazi za kilimo, uchimbaji madini ya shaba, na utalii ili nchi hiyo itapata maendeleo ya uchumi mbalimbali.
"Botswana inategemea mapato ya almasi, si kama tu imepata nguvu bora, lakini hii pia imeonesha udhaifu wake. Ili kuhakikisha mustakabali wa Botswana, ni lazima kuendeleza uchumi wa sekta muhimu kama vile utalii, kilimo, viwanda, teknolojia ya habari na huduma ya afya," Gaolathe ambaye pia ni waziri wa fedha wa nchi hiyo amesema, wakati akiwasilisha bajeti ya kwanza ya Bunge la 13 katika mji mkuu wa Gaborone.
Gaolathe amesema kuwa kuendeleza kazi ya uchimbaji wa madini mbalimbali na kufuatilia zaidi kazi ya kuchagua madini ni nguzo kuu za mkakati wao.
“Kampuni kama vile Kampuni ya Mgodi wa Shaba wa Khoemacau, itanunuliwa na mfanyabiashara wa uchimbaji madini wa China kwa dola za Marekani bilioni 1.88, na itafanya kazi muhimu katika kushughulikia ukosefu wa ajira,” amesema.
Ameongeza kuwa, kampuni hiyo inaanza mradi wa upanuzi utakaoongeza uzalishaji wa shaba kutoka tani 60,000 hadi angalau tani 130,000 kwa mwaka, ikiongeza nguvu kazi kutoka 2,000 hadi 4,000.
“Juhudi zaidi za kuendeleza uchumi mbalimbali ni pamoja na kuendeleza uzalishaji wa mbegu, kuanzisha viwanda vya mbolea ili kupunguza hali ya kutegemea kuagiza bidhaa kutoka nje, na kuifanya sekta ya umeme kuwa ya kisasa kwa kupitia kutumia nishati ya jua kuwa nishati kuu ya nchi hiyo” Gaolathe ameeleza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma