

Lugha Nyingine
Nchi za Afrika zahimizwa kuongeza uwekezaji katika elimu ya wasichana
Nchi za Afrika zimehimizwa kuhakikisha usawa wa kijinsia katika elimu huku wito ukitolewa wa kuongeza uwekezaji katika elimu ya wasichana katika bara zima.
Wito huo umetolewa na wataalamu na watunga sera waliohudhuria mdahalo wa ngazi ya juu kuhusu usawa wa kijinsia katika elimu, uliofanyika Jumanne kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia, ukiwa na kauli mbiu "Kuwekeza katika Mifumo ya Elimu ya Wasichana kama Njia ya Fidia, Haki, na Maendeleo Endelevu kwa Jamii za Afrika."
Mjadala huo uliofanyika kando ya mkutano wa 38 wa AU wa mwaka huu, umetathmini hali ya elimu ya wasichana barani Afrika.
Mkutano huo umesisitiza ulazima wa kuwekeza katika elimu ya wasichana kama njia ya haki na chombo cha maendeleo, ikienda sambamba na kaulimbiu ya mwaka 2025 ya AU: "Haki kwa Waafrika na Watu Wenye Asili ya Afrika Kupitia Fidia."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma