

Lugha Nyingine
Wadau wa Afrika wanaojadili mabadiliko ya tabianchi wakutana nchini Kenya ili kuhimiza haki ya tabianchi
Wadau zaidi ya 70 wa Afrika wanaojadili mabadiliko ya tabianchi wamekutana mjini Nairobi nchini Kenya kwenye Mkutano Maalum cha siku mbili wa Kundi la Afrika la Wadau wa Mabadiliko ya Tabianchi ili kuhimiza haki ya tabianchi barani humo.
Mkutano huo uliohudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 35 za Afrika, kinalenga kujadili msimamo mmoja wa Afrika kuhusu ufadhili wa tabianchi, mwitikio wake, hasara na uharibifu, na kuhakikisha kuwa sauti ya bara hilo inaendelea kuwa imara katika mazungumzo ya tabianchi duniani.
Mjumbe maalum wa tabianchi wa Kenya na mwenyekiti wa Kundi la Afrika la Majadiliano ya Mabadiliko ya Tabianchi, Ali Mohamed, amesema mkutano huo umekuja wakati muhimu kwa ajenda ya tabianchi ya Afrika kwa sababu watapitia matokeo ya mkutano wa 29 Nchi Watia Saini (COP29) kwa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi ambao ulifanyika Baku, Azerbaijan, Novemba 2024.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma