

Lugha Nyingine
Rais wa Kenya ahimiza juhudi za kuibadilisha Afrika kuwa bara lenye nguvu duniani
Rais William Ruto wa Kenya ametoa wito kwa viongozi wa Afrika kuzidisha juhudi ili kutimiza haraka Ajenda ya 2063, ambayo ni mwongozo na mpango mkuu wa Afrika, kwa ajili ya kuligeuza bara hilo kuwa nguvu kuu ya kimataifa ya siku zijazo.
Akiongea kwenye mkutano wa mtandaoni Jumatatu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika na Ushirikiano Mpya wa Maendeleo ya Afrika (AUDA-NEPAD) kwa Wakuu wa Nchi na Kamati ya Maelekezo ya Serikali, Rais Ruto amesema mafanikio ya Ajenda ya 2063 hayategemei bahati au matumaini, bali ni chaguo, azimio na utekelezaji usiokoma.
Ameongeza kuwa wanapaswa kukusanya rasilimali, kuimarisha utawala, na kuunda ushirikiano unaoleta matokeo halisi kwa watu wa Afrika.
Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya rais iliyotolewa mjini Nairobi, Rais Ruto amesema uongozi wa bara la Afrika una jukumu la kuweka mwelekeo wa maendeleo endelevu ya Afrika kwa kuingiza, kutekeleza na kutetea Ajenda 2063.
Amesema, mpango huo una uwezo si tu wa kusaidia baadhi ya nchi bali pia kuibadilisha Afrika kwa ujumla.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma