China yaionya Ufilipino juu ya hatari ya uwekaji wa muda mrefu wa mfumo wa makombora wa Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 13, 2025

BEIJING - China imeihimiza Ufilipino kutimiza ahadi yake ya kuondoa mfumo wa makombora wa Typhon wa Marekani kutoka kwenye ardhi yake, ikionya kwamba kutofanya hivyo kutaweka usalama na ulinzi wake wa taifa katika uchezaji wa wengine, na kutaleta hatari ya makabiliano ya siasa za kijiografia na mashindano ya silaha katika kanda.

Guo Jiakun, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China amesema hayo jana Jumatano kwenye mkutano na waandishi habari wakati akijibu swali husika.

Amesema kuwa, Marekani iliweka mfumo huo wa makombora wa Typhon kaskazini mwa Ufilipino mwezi wa Aprili 2024 ikiwa ni sehemu ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Ufilipino na kwamba Ufilipino iliahidi kuwa uwekaji huo utakuwa "kwa muda," na kwamba mfumo huo utaondolewa baada ya kukamilika kwa mazoezi hayo ya kijeshi.

“Hata hivyo, Ufilipino mara kwa mara imekwenda kinyume cha ahadi yake hiyo na hata inapanga "kununua" mfumo huo ili kuongeza uwezo wake wa kuzuia mashambulizi. Pia imeunganisha Bahari ya Kusini na mfumo huo wa makombora katika hatua hii ambayo ni "ajabu na hatari," Guo amesema.

Amesema kuwa Typhon ni silaha ya kimkakati, ni ya mashambulizi yenye masafa yanayoweza kufika nchi nyingine za Asia Kusini-Mashariki, akiongeza kuwa uwekaji huo wa Marekani wa mfumo wa makombora nchini Ufilipino unadhoofisha sana amani na utulivu wa kikanda na kuathiri maslahi halali ya usalama ya nchi nyingine.

“China kamwe haitakaa kimya kwani maslahi yake ya usalama yanahatarishwa au kutishiwa, na nchi nyingine katika kanda hii hazitakubali hatua hiyo potovu,” Guo amesema.

Ameihimiza Ufilipino kufanya chaguo la kimkakati ambalo linatumikia kwa dhati maslahi ya kimsingi ya Ufilipino na watu wake. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha