

Lugha Nyingine
Bustani kubwa zaidi ya barafu na theluji duniani mjini Harbin yavutia watalii wengi
![]() |
Picha ikionyesha watalii wakitembelea Bustani ya Barafu na Theluji ya Harbin mjini Harbin, Mkoani Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Januari 23, 2025. (Xinhua/Zhang Tao) |
HARBIN – Bustani ya Barafu na Theluji ya Harbin, bustani kubwa zaidi yenye kauli mbiu ya barafu na theluji duniani, imekaribisha watu zaidi ya milioni 3 walioitembelea hadi kufikia Jumanne wiki hii, ikiweka rekodi mpya ya idadi ya watalii waliotembelea katika siku 52 tu tangu kufunguliwa kwake kwa mwaka wa 26, waandaaji wametangaza.
Ikiwa inapatikana Harbin, mji mkuu wa Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini-mashariki mwa China na mara nyingi ukitajwa kwa jina la "mji wa barafu," mwaka huu bustani hiyo imejengwa kwa barafu na theluji zenye mita za ujazo 300,000 na ina miundo fafanuzi ya barafu iliyohamasishwa na Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia unaofanyika mjini humo.
Zaidi ya sanamu zake za kisanii za barafu, bustani hiyo inatoa vivutio vingi vya majira ya baridi, ikiwa ni pamoja na safu za barafu zenye njia za theluji, miteremko ya kwenye barafu, na njia kubwa za kutereza kwenye barafu zikikamilishwa na ndogo zaidi ya 20.
"Kuna baridi kali ya kugandisha, lakini inafurahisha sana! Wakati wa mchana, sanamu za barafu zinameta kama fuwele, na usiku, taa zinazometa hubadilisha bustani hiyo kuwa eneo la ajabu la majira ya baridi," Mandizvidza Shalom Zivo, mtalii kutoka Zimbabwe amesema.
Bustani hiyo ina ukubwa wa mita za mraba milioni 1, ikipanuka kutoka mita za mraba 800,000 za mwaka jana. Hii ni bustani kubwa zaidi katika historia yake ya miaka 26.
Ikiwa ni bustani yenye kauli mbiu ya barafu na theluji iliyojiimarisha, Bustani ya Barafu na Theluji ya Harbin inajulikana kuwa moja ya vivutio vya China vya majira ya baridi. Ilipata umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii ya China msimu wa baridi uliopita, ikawa kivutio cha kwenye intaneti wakati ambapo shauku ya michezo ya msimu wa baridi na utalii ikiendelea kuongezeka kote nchini humo.
China inalenga kuinua uchumi wake wa barafu na theluji kama chanzo kipya cha ukuaji, ikilenga kiasi cha kiuchumi cha yuan trilioni 1.2 (sawa na dola za kimarekani bilioni 167.34) ifikapo mwaka 2027 na yuan trilioni 1.5 ifikapo mwaka 2030, kwa mujibu wa miongozo iliyotolewa na Baraza la Serikali la China mwaka jana.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma