CGCC yasherehekea maadhimisho ya miaka 20 ya kukuza biashara kati ya Marekani na China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 13, 2025
CGCC yasherehekea maadhimisho ya miaka 20 ya kukuza biashara kati ya Marekani na China
Watu wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Sherehe ya Utambuzi wa "Ishirini kwa Ishirini" kuenzi safari ya ajabu ya miaka ishirini ya Shirikisho Kuu la Wafanyabiashara wa China nchini Marekani (CGCC), kwenye shughuli ya maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa CGCC katika Jiji la New York, Marekani, Februari 11, 2025. (Xinhua/Li Ruhua)

NEW YORK – Likifikisha miongo miwili ya kukuza ushirikiano wa kiuchumi, Shirikisho Kuu la Wafanyabiashara wa China nchini Marekani (CGCC) na Mfuko wa CGCC limeandaa shughuli kubwa ya maadhimisho ya miaka 20 katika Jiji la New York, Marekani siku ya Jumanne lenye kaulimbiu ya "Kujenga mawasiliano na Kutengeneza Fursa".

Sherehe hiyo, iliyokusanya watendaji wakuu, maafisa wa serikali, na viongozi wa fikra 300, imeadhimisha miongo miwili ya dhamira isiyoyumba ya CGCC ya kupanua ushirikiano na fursa kati ya jumuiya za wafanyabiashara za Marekani na China.

"Katika kipindi chote cha miongo miwili iliyopita, CGCC imekua kutoka muungano mdogo wa kampuni zenye maono hadi kuwa shirikisho la wafanyabiashara linalojitegemea na lenye mchango mkubwa zaidi, lisiloegemea upande wowote, na lisilo la kiserikali linalounganisha jumuiya za wafanyabiashara wa Marekani na China," amesema mwenyekiti wa CGCC Hu Wei, ambaye pia ni Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya China Marekani katika hotuba yake ya ufunguzi.

"Dhamira yetu ya kujenga thamani, kuhimiza ukuaji wa uchumi, na kuimarisha ushirikiano wa pande mbili haijawahi kuyumba. Kaulimbiu ya jioni hii -- Kujenga mawasiliano, Kutengeneza Fursa -- inanasa kiini halisi cha dhamira yetu na matarajio yetu pamoja ambayo yanatuunganisha," Hu amesema.

Michael R. Bloomberg, mwanzilishi wa Bloomberg LP na Shirika la Hisani la Bloomberg na meya wa zamani wa New York City, ametoa ujumbe maalum wa video akipongeza CGCC kwa kuadhimisha miaka 20.

Bloomberg amepongeza juhudi za CGCC katika kuhimiza ushirikiano wa kibiashara kati ya Marekani na China na kusisitiza jukumu lake lisilo na mbadala katika kukuza uhusiano mzuri kati ya pande hizo mbili.

Ametoa shukrani kwa kampuni zilizohudhuria kwa mchango wao katika biashara, usalama na mabadiliko ya tabianchi, na kusisitiza tena dhamira ya Bloomberg ya kuunganisha China na masoko ya fedha ya kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha