

Lugha Nyingine
Trump asema Marekani na Russia zitaanza mazungumzo kumaliza mgogoro wa Ukraine mara moja
Rais Donald Trump wa Marekani akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Januari 30, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)
WASHINGTON - Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba yeye na Rais Vladimir Putin wa Russia wamekubaliana katika mazungumzo kwa njia ya simu mapema jana Jumatano kwamba nchi hizo mbili zitaanzisha mara moja mazungumzo ya moja kwa moja yenye lengo la kumaliza mgogoro kati ya Ukraine na Russia.
"Nimefanya mazungumzo ya simu ya muda mrefu na yenye matokeo na Rais Vladimir Putin wa Russia," Trump amesema, akitoa sehemu yake ya maudhui ya mazungumzo hayo ya simu katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa Truth Social.
Trump amesema yeye na Putin wamekubaliana kwamba "tunataka kukomesha mamilioni ya vifo vinavyotokea katika Vita kati ya Russiana Ukraine."
"Tumekubaliana kushirikiana kwa karibu, ikiwemo kufanya ziara katika nchi za kila mmoja. Pia tumekubaliana timu zetu husika zianze mazungumzo mara moja, na tutaanza kwa kumpigia simu Rais Zelenskyy wa Ukraine, kumfahamisha kuhusu mazungumzo haya, nitalifanya hilo sasa hivi," Trump amesema.
Ameeleza kuwa amewaagiza Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, Mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la Marekani (CIA) John Ratcliffe, Mshauri wa Usalama wa Taifa Michael Waltz na Mjumbe Maalum wa Mashariki ya Kati Steve Witkoff kuongoza timu ya Marekani kwenye mazungumzo hayo.
Trump amesema anahisi "sana" kwamba mazungumzo hayo kati ya Marekani na Russia "yatafanikiwa."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma