Chama cha upinzani cha Sudan Kusini chapinga kufutwa kazi serikalini kwa maafisa wake

(CRI Online) Februari 13, 2025

Chama cha upinzani cha Sudan Kusini cha Sudan People's Liberation Movement-in-Opposition (SPLM-IO), kinachoongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar, kimetoa wito wa kurejeshwa kazini kwa maafisa wawili wa chama hicho ambao walitimuliwa kwenye serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa na Rais Salva Kiir.

Waziri wa Afya Yolanda Awel Deng, na Gavana wa Jimbo la Ikweta Magharibi Alfred Futuyo Karaba ni miongoni mwa maafisa tisa waliofutwa kazi chini ya amri ya rais iliyosomwa kwenye Shirika la Utangazaji la Sudan Kusini.

Katika taarifa yake hiyo siku ya Jumatano, Machar amekataa kile alichokiita "uamuzi wa upande mmoja" wa rais kuwafuta kazi maafisa hao, akikiuka Mkataba wa Amani wa 2018, ambao pamoja na mambo mengine umeweka sharti la kufanya maamuzi ya pamoja kati ya pande zilizotia saini kabla ya kufanya mabadiliko makubwa ndani ya serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha