Mtaalamu wa Tanzania achaguliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa ECSA-HC

(CRI Online) Februari 13, 2025

Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya nchini Tanzania Ntuli Kapologwe, amechaguliwa kuwa mkurugenzi Mkuu Mpya wa Jumuiya ya Afya ya Afrika ya Mashariki, Kati na Kusini (ECSA-HC), shirika linalojikita katika kuhimiza ushirikiano wa afya wa kikanda kati ya nchi wanachama.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya ya Tanzania jana Jumatano, Ntuli Kapologwe amechaguliwa katika nafasi hiyo baada ya kuwashinda wenzake sita kwenye uchaguzi uliofanyika nchini Malawi.

Waziri wa Afya wa Tanzania Jenista Mhagama amesema hii ni mara ya pili kwa Tanzania kuchukua nafasi hiyo kwenye ECSA-HC ambapo wa kwanza alikuwa Winnie Mpanju aliyetumikia kuanzia mwaka 1993 hadi 2000.

Mhagama ameongeza kuwa ushindi huo unaonyesha kuwa Tanzania inaendelea kutambuliwa kwenye jukwaa la kimataifa, ikiwa na wataalamu bingwa wanaoweza kuongoza mashirika ya kimataifa na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya afya duniani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha