Mkuu wa Mawaziri wa Kenya atoa wito wa kufanyika mazungumzo ili kutatua mgogro mashariki mwa DRC

(CRI Online) Februari 13, 2025

Mkuu wa Mawaziri wa Kenya Musalia Mudavadi, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora ametoa wito wa kufanyika kwa "mchakato wa mazungumzo" ili kushughulikia mgogoro unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Akihudhuria Mkutano Mkuu wa 46 wa Kawaida wa Baraza la Utendaji la Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia, Mudavadi amewaambia wanahabari kuwa usimamishaji vita "bado haujafikiwa kikamilifu" na unaweza kufikiwa kwa mazungumzo tu.

Mudavadi amesema kuwa mapigano yameanza tena katika baadhi ya maeneo nchini DRC, akisisitiza kwamba kurejesha amani siyo "suala la mgawanyiko" bali ni mchakato unaohitaji mazungumzo na pande husika na kuelewa hali tete ya eneo hilo.

Waziri huyo amesema kuwa hatua muhimu, zikiwemo Mchakato wa Luanda na Nairobi, zimechukuliwa ili kupunguza hali ya wasiwasi katika eneo hilo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha