

Lugha Nyingine
Kenya yaimarisha hatua za kuzuia kuenea kwa magonjwa yanayoambukizwa na virusi
Mamlaka ya afya ya Kenya imesema kuwa hatua madhubuti zinaendelea kuchukuliwa ili kupunguza hatari za magonjwa yanayoambukizwa na virusi kama vile Marburg, mpox, na Ebola kote nchini humo.
Waziri wa Afya wa nchi hiyo Deborah Barasa amesema siku ya Jumatano kwamba ingawa mlipuko wa virusi vya Marburg bado umedhibitiwa katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, lakini ukaribu wa kijiografia wa Kenya na mwingiliano mkubwa wa mipaka unasababisha hatari kubwa ya watu wenye virusi hivyo kuingia nchini humo.
Barasa amesema Wizara ya Afya, kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) na washirika wengine, imeongeza hatua za ufuatiliaji na mwitikio ili kuhakikisha kuwa kuna maandalizi endelevu.
Ameongeza kuwa juhudi pia zinaendelea kuwezesha upatikanaji wa chanjo dhidi ya mpox kupitia ushirikiano na WHO na Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma