

Lugha Nyingine
Umoja wa Afrika kuchagua mwenyekiti mpya
(CRI Online) Februari 14, 2025
Nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika zimekutana leo Ijumaa mjini Addis Ababa, Ethiopia, kwa ajili ya kumchagua mwenyekiti mpya wa Umoja huo.
Mkutano huo unatarajiwa kuwa na mjadala mzito, ukikutanisha wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.
Kabla ya mkutano mkuu, viongozi hao watafanya kikao cha dharura kujadili machafuko yanayoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambapo waasi wa M23 wanakalia maeneo muhimu baada ya kushinda majeshi ya serikali.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma