

Lugha Nyingine
Sudan yatoa wito kwa AU kutengua kusimamishwa uanachama wake
(CRI Online) Februari 14, 2025
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesema kuwa Sudan imetoa wito kwa Umoja wa Afrika (AU) kutengua kusimamishwa uanachama wa nchi hiyo.
Taarifa hiyo imesema kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Ali Yousif Ahmed aliwatumia barua mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama katika Baraza la Amani na Usalama la AU (AUPSC), kabla ya mkutano wa baraza hilo uliopangwa kufanyika leo Ijumaa mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia.
Waziri huyu wa Sudan amelitaka baraza hilo kuangalia upya tathmini ya AU juu ya hali ya Sudan, akisisitiza haja ya Sudan kurejea kwenye nafasi yake halali ndani ya shirika la bara hilo na kuanza tena jukumu lake katika masuala ya Afrika.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma